Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa siku kadhaa zilizopita amekuwa katika wakati mgumu na kushindwa kuelewa neno gani anaweza kumpa Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, John Heche kufuatia kifo cha mdogo wake Suguta ambaye alifariki kwa kuchomwa kisu na askari.

Amesema kuwa kifo ambacho kilimpata mdogo wake Heche kinaumiza sana ndiyo maana kwa siku kadhaa amekosa maneno mazuri ya faraja kumpa kiongozi huyo wa CHADEMA.

“Nimefikiria kwa muda mrefu, maneno gani nitumie kukupa pole lakini imeniwia vigumu sana kuyapata maneno hayo kutokana na aina ya kifo kilichokatisha maisha ya kijana mdogo kabisa katika Taifa,”amesema Mbowe

Hata hivyo, Mbowe ametumia wakati huo kutoa pole kwa familia ya John Heche kufuatia kifo cha mdogo wake huyo.

Furahia wikendi yako na video hii kutoka kwa Ngoma wa Cameroon
Wanaume watakiwa kujitokeza kupima Ukimwi