Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi na kupokelewa na mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt. John Magufuli.

Akizungumza wakati wa kumpokea Lowasa, Rais Magufuli amesema kuwa kiongozi huyo alikwenda CHADEMA kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake, hivyo kaamua kurudi nyumbani CCM kwaajili ya kuendelea kukitumikia chama chake.

“Ndugu yetu amerudi na ametueleza sababu zilizomuondoa kuwa zilikuwa nje ya uwezo wake”, amesema Rais Dkt. Magufuli.

Aidha amesema kuwa baada ya kutafakari kwakina ameamua kurejea nyumbani, hivyo wameamua kumpokea ili aweze kuungana na wanachama wenzie wa Chama Cha Mapinduzi.

Lowassa alitimkia CHADEMA mwaka 2015 baada ya kukatwa jina lake na Kamati Kuu ya CCM katika kinyang’anyiro cha kugombea Urais.

 

Sumaye azungumzia uwezekano wa kurudi CCM
Sirro aomba msaada kwa viongozi wa dini, 'Mtusaidie jamani'