Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Msigwa amekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa gari yake inauzwa kutokana na hali ngumu ya maisha.

Katika mtandao wake wa kijamii, Msigwa ameweka picha ya gari hilo na namba za gari hilo na kuandika kuwa “Gari hili la Mh. Msigwa haliuzwi”

Akizungumza na mwandishi wa habari wa Dar24Media kwa njia ya simu, Msigwa amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote, hivyo zinapaswa kupuuzwa.

“Subiri nikwambie kitu kimoja, kwani wewe unajua kuna vitu vingapi mimi nimeuza, nakwambia hizo habari sio za kweli ndio maana nimekanusha,”amesema Msigwa

Aidha, katika taarifa za awali zilizokuwa zimeenea kwenye mitandao ya kijamii zimesema kuwa Msigwa alitangaza kuuza gari yake kutokana na hali ngumu ya kimaisha iliyopo kwasasa.

 

 

 

 

 

Shirika la Amnesty International laonya hatua za RC Makonda
LIVE DODOMA: Makamu wa Rais katika uzinduzi wa Tamasha la MVINYO Dodoma

Comments

comments