Mbunge wa jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amesema kuwa amesikitishwa sana na kitendo cha polisi mwenye namba E1156 Koplo William Marwa ambaye anadaiwa kufanya mauaji kwa mdogo wa Heche.

Ameyasema hayo mara baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya kudai kuwa linamshikilia polisi huyo kwa tuhuma za kumchoma kisu, Chacha Heche Suguta ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche.

“Kitendo kilichotokea sio tu kimesikitisha ukoo wa Heche lakini kwangu binafsi. Jeshi letu limetengenezwa kulinda watu na mali zao sio kuumiza wasio na hatia. Ni imani yangu Serikali itasimamia haki kwa familia ya Heche. Poleni sana kwa msiba. Mungu awape subira John Heche,”amesema Ridhiwani

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, Henry Mwaibambe amethibitisha kumshikilia askari wake mwenye namba E1156 Koplo William Marwa kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Suguta Chacha mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa Sirari wilayani Tarime mkoani Mara kwa kumchoma Kisu.

 

 

 

Kansela wa Ujerumani akutana na Trump
King Kibadeni awafunda wachezaji wa Simba na Yanga