Mwandishi wa Riwaya hapa Tanzania ambaye pia ni mshindi tuzo  kipengele cha Riwaya bora ya Kiswahili  kwenye tuzo za Mabati-Cornell(2020), Lello Mmasy atamani kuandika tawasifu ya waziri mkuu wa zamani Edward Lowasa.

Akizunngumza hayo kwenye mahojiano maalum na kituo cha habari cha  Dar24 , Mmasy amesema amekuwa ana adhima ya kuandika tawasifu ya mwanasiasa Edward Lowasa, lakini amekuwa anapata changamoto kadhaa kukutana na mwanasiasa huyo mashuhuri.

“Mimi ninamtafuta sana Lowasa nadhani anasimulizi nzito kidogo, mnaweza kuona ni nyepesi lakini  kisa chake ni kizuri sana namna kilivyo kwenye akili yangu nikikiwasilisha nadhani itakuwa moja ya vitabu nitakavyojivunia maisha yangu yote,” amesema Mmasy.

Aidha amesema kuwa awali alifikia hatua nzuri ya kuandika tawasifu ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia kabla ya kukamilisha lengo lake.

Katika hatua nyingine Mmasy ametangaza kuwa Februari, 2021  anatarajia kuzindua kitabu chake cha pili kiitwacho  Chochoro za Madaraka  (Alleys Of Power), ambapo amewata wasomaji wa riwaya kukaa mkao wa kusoma kazi hiyo.

Bofya hapa……..

Wahitimu watakiwa kutumia fursa ya mikopo
Bilioni 800 Kukarabati Barabara Geita