Muigizaji wa filamu za kibongo, Salma Jabu maarufu kama Nisha, amewatolea uvivu wanaume wenye tabia za kupenda kulelewa, kuhudumiwa na wanawake, amefunguka na kusema yeye binafsi ameshawahi kulea na kuhudumia wanaume wa dizaini hiyo.

Hata hivyo kwa sasa imekuwa tabia kwa wasanii wanawake wa bongo movie pamoja na wasanii wa muziki na wale waliopo kwenye urembo na mitindo kuwa na mahusiano na vijana walio na umri mdogo.

”Mimi ni miongoni mwa wanawake ambao nimekuwa na mahusiano na wanaume wanaopenda kutegemea kwa kila kitu”. Amesema Nisha.

Amesema kuwa wanaume wenye tabia hiyo wengi hawapendi kufanya kazi kwa madai kuwa wanatunzwa na wanawake walionao kimapenzi.

Nisha amezungumza hayo kwenye kipindi cha Friday Night Live ya EATV, na kuweka wazi kuwa mwanaume ambaye ni tegemezi hawezi kudumu naye na inafikia kipindi humkana kabisa mbele ya watu.

” Siyo kwamba mtu hanauwezo wa kufanya kazi lakini anataka kupewa kila kitu mimi sitowezana naye  na kama kuna mwanaume wa aina hiyo amekaa akisubiri nafasi hiyo kwangu amefeli”. amesema Nisha babe.

Aidha ameeleza pia wapo wanawake wenye tabia ya kutegemea kila kitu kwa mwanaume wakati uwezo wa kujishughulisha upo, hivyo amewasihi watu kujishughulisha na kuachana na dhana ya kuwa mzigo kwa wenzi wao, emeeleza watu inabidi wajitambue na kusaidiana inapotokea mtu ameonekana kukwama, na isiwe tabia ya kuomba omba wakati nguvu ya kufanya kazi upate chako ipo.

 

 

 

 

 

Gwajima atakiwa mahakamani Agosti 30
Video: Bi Hindu afyatuka, asema Klabu ya Simba haihitaji mabadiliko