Muongozaji wa video za muziki, Nisher ambaye baba yake ni mhubiri maarufu jijini Arusha mwenye utajiri mkubwa, ameeleza mpango wake wa kuachana na mambo ya dunia na kufuata nyayo za baba yake huyo aliyeokoka.

Akizungumza hivi karibuni katika kipindi cha Mkasi, Nisher alieleza kuwa yuko tayari kuachana na mambo yote na kuokoka…. lakini muda alioutaja unaonesha kuwa bado anataka kula ujana kwanza, wokovu baadaye sana.

Alisema kuwa ingawa wazazi wake wangependa aokoke na kufuata nyayo zao lakini hawajawahi kumlazimisha. Muongozaji huyo ambaye ni mshindi wa Tuzo za Watu, alieleza kuwa huenda akachukua maamuzi ya kuokoka akiwa na umri wa kuanzia miaka 45 hivi, hali inayoonesha kuwa kwake uzee ndio unaweza kumfanya akajisalimishe kwa Yesu na kuanza maisha mapya.

Katika hatua nyingine, Nisher alielezea kile kinachodaiwa kuwa hutumia fedha nyingi za baba yake kama fimbo ya kuwasumbua wenzake katika tasnia ya Muziki.

“Kwangu mimi mimi naposikia watu wanasema natumia fursa hiyo kufanya whatever am doing, well… kuna some truth na nyingine sio. Kwa sababu baba ni kama muwekezaji wangu, ananiwekezea chochote ambacho ningependa kukiona kinafanikiwa kama ni muziki. Kwa sababu mimi familia yetu muziki umetawala. Kuna dada anaimba, my mom na wadogo zangu wote,” alisema Nisher.

“So mimi nisingeiona sana kama natumia fedha yake kwa style hiyo. In facts, ninatumia pesa yangu hivi sasa kwa sababu ninafanya kazi hizi,” aliongeza.

Mama yake Diamond Alipata maumivu alipokuwa anashuti 'Utanipenda'
Mtibwa Sugar Kusaka Heshima Ya Watanzania Leo