Kiungo mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara timu ya Yanga, Harouna Niyonzima amesema kuwa mkataba wake na Yanga umemalizika lakini amegoma kuongelea tetesi zilizopo kuwa amesaini mkataba na timu ya Simba.

Amesema kuwa kwa sasa yupo mapumzikoni hivyo anashughulikia masuala ya familia na kwamba kwa sasa hayuko tayari kuongelea suala hilo hivyo muda ukifika kila mmoja ataelewa ni wapi anaelekea.

“Kwa sasa niko likizo hivyo, nafuatilia na kufanya shughuli za familia yangu, siwezi kuongelea kitu chochote kuhusu mkataba wangu na muda ukifika kila mmoja ataelewa ni wapi nitakapoelekea kama ni Simba au kubaki Yanga,”amesema Niyonzima

Aidha, katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na uvumi kuwa Niyonzima amesaini mkataba na timu ya Simba baada ya kumalizika kwa mkataba wake na timu ya Yanga aliyokuwa akiitumikia msimu uliomalizika.

Hata hivyo, Simba na Yanga zimekuwa zikihusishwa kuiwania saini ya Niyonzima, miongoni mwa viungo mahiri zaidi Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL)

Video: Rugemalira, Seth wa Escrow kula kulala kwa amri, IPTL moto
Magazeti ya Tanzania leo Juni 20, 2017