Licha ya kuitumikia Simba SC hadi kuwa miongoni mwa wachezaji walioifikisha klabu hiyo hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika msimu 2018/19, kiungo kutoka Rwanda Haruna Niyonzima amesema hakuwahi kuwa na fuhara Msimbazi.

Niyonzima aliemaliza mkataba wake Young Africans na kuagwa kwa heshima, amesema ilimlazimu kusajiliwa na Simba SC kutokana na changamoto alizozipitia Young Africans, lakini bado hakucheza kwa furaha kwa Mabingwa hao wa Tanzania Bara mara nne mfululizo.

“Sikuwahi kuwa na furaha nilipokuwa Simba SC, lakini sikuwa na namna, Simba na Young Africans ni klabu kubwa lakini Young Africans niliishi kama nyumbani, kuna mambo yalitokea nikalazimika kwenda Simba SC”

“Lakini maamuzi yale yalinifanya niamini kuwa kwenye maisha hela sio kila kitu” amesema Haruna bila kufafanua kwa undani kauli hiyo ya pesa.

Baada ya kuitumikia Simba SC kwa misimu miwili, Haruna alirejea nchini kwao Rwanda kujiunga na AS Kigali kabla ya kusajiliwa tena Young Africans mapema mwaka 2020.

TPLB yatoa sababu kuchelewa kumalizika Ligi Kuu
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 29, 2021