Kufanya mtu avutiwe nawe kwa mara ya kwanza kazini ni muhimu sana ndani ya wiki ya kwanza ya ajira yako. Inaweza kukutisha kidogo, kutokana mambo kadha wa kadha kama vile shinikizo la kukutana na watu wapya, kuwa na hisia zilizo katikati, kuelewa mazingira mapya ya kazi na kadhalika. Kibinadamu, hisia hizi ni za kawaida kabisa. Hupaswi kuwa na wasiwasi juu ya kukutana kwa wafanyakazi au viongozi wako.

Hivi ni vidokezo vya vitu vya kufanya ili kuwa imara katika wiki yako ya kwanza kwenye kazi yako mpya.

1.  Zingatia na Elewa Mfumo na Tamaduni Zao

Kuzingatia kwa makini mtindo wa mawasiliano na tamaduni miongoni mwa wafanyakazi wenzako ni mwanzo mzuri wa kukabiliana na kazi yako mpya. Ni muhimu kuelewa mwingiliano baina ya wafanyakazi wenzako, ni nani utakayemfata wakati una maswali na ni muhimu kujua majina ya watu ambao utakutana nao. Hakikisha unasoma nyaraka na kuwa unatambua na kuandika pembeni kila kitu muhimu unachojifunza.

    2. Jipange

Wiki ya kwanza pia ni wakati mzuri wa kuhakikisha utambua vitu muhimu ambavyo vinasaidia mtiririko wako wa kazi. Anza kwa kuandaa meza yako, saini yako ya barua pepe, akaunti za mitandao ya kijamii na hakikisha una mawasiliano ya watu wote muhimu ofisini. Pia, hakikisha unafahamu maeneo muhimu kama vile sehemu za kupumzikia, eneo la chakula cha mchana na huduma zingine zinazopatikana ndani ya ofisi yenu. Zaidi ya hayo, hakikisha unapima safari yako ili ujue muda sahihi wa kuondoka nyumbani na njia za usafiri utakayotumia ili kuepuka kuchelewa kazini.

    3. Jenga Mahusiano

Kuwa na mahusiano na wafanyakazi wenzako kutasaidia kuwa na ujasiri utakapoanza kazi yako mpya. Tafuta muda sahihi utoe utambulisho mfupi na waharaka kwa watu wapya ambao unakutana nao. Unaweza usipate rafiki wako wa kudumu hapo, lakini ukapata mtu ambaye mnaweza kuendana na akakupa utulivu utakaohitajika. Ni muhimu kuwa na marafiki katika hatua hii ili kukusaidia katika kuwa ujasiri na utendaji mzuri kazini. Tafiti iliochapishwa katika jarida la Journal of Business and Psychology unaonyesha kwamba urafiki mahali pa kazi una faida za moja kwa moja kwa wafanyakazi na utendaji kazi, kuridhika kufanya kazi hiyo pamoja na faida ya moja kwa moja juu ya kujitolea katika shirika.

     4. Uliza Maswali Mengi Iwezekanavyo

Ili kujifunza haraka katika mazingira yako mapya ya kazi, utahitajika kuwasiliana na viongozi wako na wafanyakazi wenzako mara nyingi iwezekanavyo. Tenga kabisa mambo muhimu unayohitaji kujua, kama swali, ushauri au kuruhusiwa kufanya kitu fulani na uliza kwa wakati fulani bila kupoteza muda. Kumbuka kuandika maswali yako ili usisahau na kuuliza yote pamoja ili kuepuka nenda rudi. Pia, unaweza kutafuta majibu ya maswali yako kwanza kupitia mitandao kama vile Google au Youtube kabla ya kwenda kuuliza ili kuokoa muda.

    5. Toa na Kubali Msaada Wao

Onyesha nia ya kujenga uhusiano mzuri na wafanyakazi wenzako kwa kujitolea kuwasaidia katika kazi zao wakati wowote watakapohitaji. Hii itakuwezesha kujifunza na kupata ufahamu juu ya jinsi mambo yanavyofanyika. Ikiwa wataamua kukupa msaada kwa kazi unayofanya, mara zote pokea msaada wao kwa mikono miwili hata kama una uwezo wa kufanya kazi hiyo yote mwenyewe. Hii itaunda uhusiano bora kati yako na wao na uwezekano wa kujifunza njia rahisi ya kukamilisha kazi zako.

   6.  Weka Malengo na Mjulishe Bosi Wako

Mwisho, wiki yako ya kwanza ni wakati mzuri wa kuweka malengo na kujua nini hasa Bosi wako anataka kutoka kwako. Hii itakuwezesha kujua mwelekeo sahihi na kasi ya kufikia malengo yako. Wakati wa mikutano ya moja kwa moja na bosi wako, tumia wakati huu kumjulisha kuhusu unayojifunza, watu unaokutana nao na changamoto unazozikabili. Pia hakikisha kwamba unaelewa malengo yako na jinsi ufanisi wa kazi zako unavyopimwa.

 

Bilioni 133.2 zimekwishalipwa kwa wakulima wa Korosho - Hasunga
Mwalimu wa Chadema atiwa mbaroni