Msuguano kati ya sehemu mbili kwa muda mrefu, unene kupita kiasi, matumizi ya deodorant, spray, matumizi ya dawa za kunyolea, matumizi ya vipodozi vikali na ugonjwa wa kisukari ni baadhi ya visababishi kwa maeneo kadhaa ya mwili kupata weusi hasa katika mapaja na kwapa, hii ni kwa wanaume na wanawake kwasababu matumizi ya vitu hivyo huchangia seli kufa kwa kiasi kikubwa na kutengeneza weusi.

Ifahamike kwamba weusi mapajani au makwapani sio ugonjwa bali ni mabadiliko tu ya ngozi ambayo huwapata wengi na kuwafanya wasiwe na raha pindi wavaapo nguo za wazi.

Zifuatazo ni baadhi ya njia za asili ambazo mhanga wa tatizo hili anaweza kuzitumia kuondokana nalo ambalo limekuwa changamoto kwa watu wengi.

  1. Mchanganyiko wa machungwa na asali ni moja ya njia salamainayoweza kusaidia kuodoa weusi huo katika mapaja na kwapwani, chakufanya chukua ganda la chungwa na kijiko cha asali kamua hnilo ganda, maji yake yaingize kwenye asali kisha kausha na kusaga hilo ganda, ukishasaga changanya unga na asali, kisha paka mchangayiko huo sehemu yenye weusi kaa kwa dakika 15 kisha jisafishe kwa maji safi hadi kuganda ganda kupotee, inashauriwa kufanya hivyo mpaka utakapoona mabadiliko ya eneo la mwili wako liliathiriwa na weusi.
  2. Njia nyingine ni matumizi ya mafuta ya nazi, mafuta haya ni tib anzuri sana kutokana na uwepo wa vitamini E yansaidia kusafisha na Kung’arisha ngozi, hivyo unachotakiwa kufanya ni kupaa mafuta hayo sehemu ya mwili iliyoathirikana weusi kwa muda wa dakika 10 hadi 20 kisha osha eneo hili kwa maji ya vuguvugu, fanya hivyo kila siku mpaka utapoona mabadiliko.
  3. Matumizi ya Tango pia ni muhimu kwa kusaidia kuondoa weusi sehemu za mapajani na kwapani, unachotakiwa kufanya, kata vipande kadhaa vya tango jipake kwapani na mapajani au lisage kisha paka ukishapaka kaa kwa muda wa dakika 10 hadi 20.
  4. Majani ya Aloevera, chukua utomvu wa jani la Aloevera, Paka kwenye sehemu yenye weusi na kisha acha ule utomvu kwa muda takribani nusu nasaa kisha osha na maji ya uvugu vugu/moto  Fanya hivi mara moja hadi mbili kwa siku ili kuweza kupata matokeo haraka.

Usitegemee mabadiliki ya ngozi yako kutokea ndani ya kipindi kifupi ni zoezi ambalo ni endelevu hivyo inashauriwa kuafnay kila siku kadri iwezekanavyo mpaka utakapopata matokeo unayoyatarijia.

 

Ridhiwani: Mambo yamebadilika, sio kama enzi za JK (Video)
Hatma ya Mbowe na wenzake kujulikana julai 2 mwaka huu

Comments

comments