Michezo ya kwanza ya nusu fainali ya Capital One Cup, ambalo ni Kombe la Ligi huko England, itachezwa hii leo Jumanne Usiku .

Leo Jumanne Stoke City watakuwa nyumbani Britannia kuwakaribisha Liverpool na kesho Jumatano Everton watakuwa Goodison Park na Man City.

michezo ya nusu fainali ya michuano hiyo itachezwa kwa mikondo miwili ya nyumbani na ugenini na timu zitarudiana tena  Januari 26 na 27.

Timu ambazo zimetinga hatua ya nusu fainali ni Stoke baada ya kuibwaga Sheffield Wednesday na Liverpool kuitoa Southampton wakati Everton waliwatoa Middlesbrough na Man City wakiitupa nje Hull City.

Bingwa Mtetezi wa Kombe hili alikuwa Chelsea ambae alitupwa nje na Stoke City kwa Mikwaju ya Penati 5-4 baada ya Sare ya 1-1.

Ni Zamu Ya Mbilinge Mbilinge Ya Kombe La FA England
Chris Gayle Aadhibiwa Kwa Kumtongoza Mwanahabari