Timu ya Njombe Mji ya mjini Njombe hatimaye imefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya timu ya Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara katika uwanja wa Nyumbani sabasaba na kuibuka na alama tatu muhimu.
Mabao ya Njombe Mji yamefungwa mnamo dakika ya 35 kipindi cha kwanza na mchezaji, Notkely Masasi huku Ahmed Tajdin akiipatia timu hiyo goli la pili katika dakika ya 61cha pili.
Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo kocha msaidizi wa Njombe Mji, Mrage Kabange amesema mchezo ulikua mzuri na la muhimu ilikua na kubakiza alama tatu uwanja wa nyumbani.
Njombe Mji walau imeonekana kukata kiu ya mashabiki wake kwani walikuwa wakisubiri kwa muda mrefu huku hofu kubwa ikiwa ni kushuka daraja.
Ushindi huo unaifanya Njombe Mji ifikishe pointi 22 baada ya kucheza mechi 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 15 kutoka ya mwisho, ikiwa mbele ya Maji Maji ya Songea yenye pointi 20 za mechi 25.
Aidha, baada ya kichapo hicho, Ndanda FC inabaki nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu ya timu 16 ikiwa na pointi zake 23 za mechi 22, nyuma ya Mbao FC yenye pointi 24 za mechi 25.
Nayo Mbeya City imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Singida United Uwanja wa Sokine mjini Mbeya katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Aprili 27.
Ligi Kuu itaendelea leo Aprili 28 kwa mechi tatu, Azam FC wakiwa wageni wa Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro, Majimaji FC wakiwakaribisha Ruvu Shooting FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songe na Stand United FC wakiwa wenyeji wa Kagera Sugar FC uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

King Kibadeni awafunda wachezaji wa Simba na Yanga
Video: Magufuli acharuka, Kikwete aungana na Mkapa janga la elimu