Serikali ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza imerusha tena lawama zake kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa madai ya kuwatunza watu waliojaribu kuipindua, Mei 2015.

Rais Nkurunzinza amerusha tuhuma hizo alipokuwa akieleza sababu za kutohudhuria mkutano wa nchi za Afrika ambao viongozi wa nchi 44 walisaini makubaliano ya kuifanya sehemu hiyo kuwa eneo huru la biashara.

“Rwanda inawatunza watu waliopanga mapinduzi na magaidi walioshirikiana kuchukua uhai wa warundi, Mei 2015,” alisema Nkurunzinza.

Katika barua yake iliyosainiwa Machi 14 ya majibu kwa mwaliko alioupokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki, Rais Nkurunzinza alimueleza kuwa angependa kushiriki mkutano huo lakini eneo la mkutano (Rwanda) ni kikwazo kwake.

 

Alieleza kuwa Rwanda imevunja mkataba wa kimataifa kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi  na silaha wakimbizi kutoka Burundi.

Mahakama nchini Kenya yamkingia kifua Miguna
Miguna aendelea kuzuiliwa uwanja wa ndege Nairobi