Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliye ripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa.

Inadaiwa kuwa alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka usingizini na kuwauliza wenyeji wa eneo alilo jikuta kuwa yuko wapi, ambapo walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa kituo cha polisi.

Aidha, Abdul Nondo alionekana kwa mara ya mwisho Jumanne katika Ofisi za Tahliso jijini Dar es salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa imetolewa na Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini Tanzania.

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) ulisema baada ya kuondoka Ofisi hizo, Nondo alielekea chuoni na kuaga kuwa anaondoka kwenda nyumbani Madale.

Hata hivyo, kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kuwa alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa na watu wasiojulikana wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimpatia vitisho.

Video: Utata waibuka mwanafunzi UDSM kupotea, Nape akoleza moto hoja ya Bashe
Mavunde awakumbuka vibarua