Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu wa Tanzania (THRDC) umemtunuku tuzo Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Omar Nondo kama mtetezi kijana chipukizi wa haki za binadamu (wanafunzi) Tanzania.

Abdul Nondo amesema kuwa tuzo hiyo kwake imekuwa na maana kubwa na kuweza kuinua hari mpya ya kuzidi kuwatetea wanafunzi katika haki zao katika masuala mbalimbali nchini na kudai tuzo hiyo imezidi kumuimarisha zaidi na kutokata tamaa na changamoto mbalimbali anazopitia katika kutetea haki za wanafunzi.

Aidha ameushukuru uongozi wa THRDC kwa kutambua mchango wa mtandao wa wanafunzi, kwani siyo kazi rahisi kutokana na changamoto nyingi ambazo anapitia katika harakati za utetezi wa haki za wanafunzi.

Amesema kikubwa katika maisha ni uvumilizu, ustahimilivu na kutambua kuwa changamoto haziepukiki katika majukumu yeyote na kutokukubali changamoto hizi kudhoofisha majukumu yake.

“Kwanza namshukuru Mwenyezimungu kwa kunipa Afya njema, pia wazazi wangu na viongozi wenzangu wa TSNP na watanzania wote kwa ujumla kwa faraja zao na matumaini yao kwangu. Napenda kutoa shukrani zangu za Dhati kwa Mtandao wa watetezi wa haki Za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kutambua mchango wetu TSNP kwa kunizawadia tuzo kama mtetezi kijana chipukizi wa haki za binadamu (wanafunzi) Tanzania nimefarijika saana” 

Aidha, Nondo ameshukuru taasisi mbalimbali za kiserikali, Wizara ya Elimu, Bodi ya Mikopo, Wizara ya Tamisemi, Tume ya Vyuo vikuu kwa kushirikiana nazo bega kwa bega katika kutetea haki za wanafunzi Tanzania.

 

Mwakyembe ataja maudhui mtandaoni ni chazo cha mmomonyoko wa maadili Tanzania
Rais Magufuli atuma salamu za pole kwa familia ya Kandoro