Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) pamoja na TSNP ulipeleka maombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumshtaki Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, IGP na Mwanasheria Mkuu.

Leo tarehe 4 Aprili 2018, Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam imeendelea kusikiliza kesi ya Mwanafunzi na mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo.

Katika kesi hiyo Mahakama ilitaka kutupilia mbali maombi ya wapeleka maombi kwani tayari kesi ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Iringa, na hivyo Mahakama Kuu kukosa mamlaka ya kuendelea na kesi hiyo.

Aidha, kufuatia uamuzi wa Mahakama kutaka kulitupilia mbali ombi hilo, Wakili wa upande wa wapeleka maombi, Mpoki aliiomba mahakama iendelee na itoe uamuzi kuhusu maombi yaliyopelekwa huku akionyesha umuhimu wa Mahakama kutoa uamuzi kuhusu maombi hayo.

Hata hivyo, baada ya kusikiliza maombi ya wakili wa upande wa wapeleka maombi, Mahakama imeamuru pande zote zifike mahakamani tarehe 11/04/2018 kwa ajili ya kusikilizwa hoja zao na baadae itatoa uamuzi.

John Bocco: Umoja na mshikamano unahitajika Msimbazi
Sababu za mwanamke kufyatulia risasi ofisi za YouTube zabainika

Comments

comments