Novak Djokovic amefuta ndoto za mkongwe wa mchezo wa tennis duniani, Roger Federer kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya Australian Open kwa mwaka 2016.

Djokovic, ambaye anaendelea kutesa kileleni mwa msimamo wa wachezaji bora wa kiume kwa viwango vya mchezo huo duniani, amefanikiwa kumchabanga mpinzani wake kutoka nchini Uswis seti tatu kwa moja ambazo ni 6-1, 6-2, 3-6 na 6-3.

Hata hivyo mchezo huo uliochezwa mjini Melbourne, ulishuhudia miamba hiyo ikipapatuana vilivyo, mpaka ilipodhidhiri Djokovic ndiye bora kuliko Federer ambaye kwa mwaka huu alionyesha kuwa na dhamira ya kutaka kurejeshwa heshima yake katika michuano hiyo.

Switzerland's Roger Federer (L) claps as he leaves the court after defeat during his men's singles semi-final match against Serbia's Novak Djokovic (R) Roger Federer akirejesha heshima kwa mashabiki wake ambao walimpigia makofi baada ya mchezo kumalizika hii leo.

Ushindi huo kwa Djokovic unaendelea kudhihirisha ahadi aliyoitoa siku chache kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, ambapo aliwaambia waandishi wa habari kwa kusema atahakikisha anajitahidi kadri awezavyo, ili akamilishe mpango wa kutetea ubingwa.

Kwa sasa Djokovic anamshubiri mshindi wa mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali unaoendelea kwa sasa kati ya Andy Murray kutoka Uingereza dhidi ya Milos Raonic, ambaye atapambana nae kwenye mchezo wa hatua ya fainali mwishoini mwa juma hili.

Serena Williams Ajiwekea Mazingira Ya Kipekee Duniani
CUF watoa Msimamo Rasmi kuhusu Ushiriki wa Marudio ya Uchaguzi Zanzibar