Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saidi (Saido) Ntibazonkiza amewataka Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kuiamini timu yao katika Michuano ya Kimataifa, licha ya kumaliza vibaya hatua ya Makundi kwa kufungwa na Raja Casablanca 3-1.

Simba SC ilicheza mchezo huo ugenini usiku wa kuamkia leo Jumamosi (April Mosi) mjini Casablanca, huku ikiwa na tiketi mkononi ya kucheza Robo Fainali kupitia Kundi C, linaoongozwa na Raja Casablanca yenye alama 16, ikifuatiwa na wababe hao wa Msimbazi wenye alama 09, Horoya AC ya Guinea imemaliza ikiwa na alama 07 na Vipers SC ya Uganda inaburuza mkia kwa kuwa na alama 02.

Saido amesema malengo makubwa ya Simba SC yalikuwa kucheza Robo Fainali na wanamshukuru Mwenyezi Mungu wamefanikiwa, hivyo wanajipanga kupambana na kufikia lengo la pili la kucheza Nusu Fainali, huku akimini hilo linawezekana kutokana na klabu hiyo ilivyojipanga.

“Malengo makubwa timu kwa msimu huu ni ya kuvuka hatua ya Robo Fainali ambayo timu imefanikiwa kucheza kwa mafanikio katika misimu ya karibuni, hivyo tunataka kwenda hatua kwa hatua, Mashabiki na Wanachama wasiwe na wasiwasi na timu yao ipo tayari kupambana.”

“Tunafahamu tutakutana na timu ngumu zaidi katika hatua hii kwa kuwa tutacheza na timu iliyoongoza kundi, lakini tunaamini kuwa tuna nafasi ya kufanya makubwa zaidi na kucheza Nusu Fainali.” Amesema Saido Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ linatarajiwa kufanya Droo ya Robo Fainali ya mashindano hayo Jumatano (April 05), ambapo Simba SC itavaana na mmojawapo wa vinara wa Kundi A, B au D.

Sally Bolo amuombea msamaha Joash Onyango
Zaidi ya Milioni 1 waathiriwa na magonjwa ikiwemo Kipindupindu