Meneja wa Tottenham Hotspur, Nuno Espirito Santo, amesema bado wachezaji wake wana imani naye, licha ya kikosi chake kuwa na matokeo mabaya katika michezo ya hivi karibuni.

Spurs imekua na matokeo yasiyoridhisha hasa baada ya kufungwa na wapinzani wao katika jiji la London Arsenal Crystal Palace pamoja na Chelsea katika michezo ya Ligi Kuu, huku wakilazimishwa sare ya 2-2 na Rennes na Wolves kwenye Ligi ya Europa Conference na Kombe la EFL.

Mwishoni mwa juma lililopita Spurs ilipoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya majirani zao wa Kaskazini mwa Jiji la London, Arsenal, matokeo ambayo yalianza kutoa ishara mbaya kwa majaliwa ya meneja huyo kutoka nchini Ureno.

Hata hivyo, Nuno, ambaye ni meneja wa zamani wa Wolves amesema wachezaji wanaamini katika mbinu zake na shutuma anazotupiwa hazimsumbui.

Akizungumza kabla ya mchezo wa jana Alhamisi dhidi ya Mura, alisema: “Ndio, kwa uhakika wananiamini sana.

“Hakuna shaka kuhusu hilo kwa sababu tunafanya kazi kwa pamoja kila siku, tunajiandaa pamoja na wachezaji wote wana imani kubwa na mimi hasa kwa mbinu zangu.”

Pep Guardiola akubali uwezo wa Donnaruma
Habari kubwa kwenye magazeti leo, October 1, 2021