Michezo ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(CHAN) inafanyika leo huko Algeria.

Katika nusu fainali ya kwanza wenyeji Algeria itakipiga dhidi Niger kwenye uwanja wa Miloud Hadefi uliopo mjini wa Oran.

Kutinga hatua hiyo Algeria imeitoa Ivory Coast wakati Niger imeiondosha Ghana.

Wawakilishi pekee kutoka eneo la Kusini mwa Afrika Mashariki, Madagascar watakuwa dimbani katika nusu fainali ya pili kuivaa Senegal kwenye uwanja wa Nelson Mandela uliopo jiji la Algiers.

Madagascar imefuzu hatua hiyo baada ya kuitoa Msumbiji wakati Senegal imeitupa nje Mauritania.

Jeshi la Polisi linanyooshewa vidole: Rais Samia
M23 Wamkimbiza Papa Francis DRC