Mabingwa wa soka nchini Hispania Real Madrid watacheza dhidi ya mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mpango wa wawili hao kukutana katika mchezo huo muhimu ambao utatoa jibu la nani ataelekea fainali ya michuano hiyo msimu huu, umefahamika baada ya kuchezeshwa kwa droo ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa leo mchana kwa saa Afrika mashariki.

Real Madrid ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano ya Ulaya, walifanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuwavurumisha Juventus FC ya Italia jumla ya mabao manne kwa matatu.

FC Bayern Munich, nao waliwafungashia virago Valencia CF ya Hispania hatua ya robo fainali kwa kuwafumnga jumla ya mabao mawili kwa moja.

Mchezo mwingine wa nusu fainali utakua kati ya majogoo wa jiji (Liverpool FC) kutoka England wamepangwa kukutana na AS Roma ya Italia.

Liverpool walifanikiwa kuitoa Man City katika mchezo wa robo fainali kwa jumla ya mabao matano kwa moja, ili hali AS Roma waliitupa nje FC Barcelona kwa jumla ya mabao manne kwa matatu.

Liverpool itaanzia nyumbani dhidi ya AS Roma huku Real Madrid ikiwa ugenini kuikabili Bayern Munich.

Mechi za mkondo wa kwanza itapigwa kati ya tarehe 24/25 Aprili 2018 huku za marudiano zikichezwa kati ya tarehe 1/2 May 2018.

Salamba mchezaji bora mwezi Machi
UEFA Europa League nusu fainali yaanikwa hadharani

Comments

comments