Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu Nairobi nchini Kenya kumjulia hali kufuatia mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.

Nyalandu amesema kuwa kwa niaba ya watu wa Singida na Watanzania wote ametoa salamu za pole kwa mke wa Tundu Lissu kwa kuwa bado hajapata nafasi ya kumuona kiongozi huyo na kusema anasubiri kama ataweza kupata nafasi ya kumuona usiku wa leo kama madaktari wataruhusu.

“Nimefika hospitali ya Nairobi mapema leo kumjulia hali Tundu Lissu madaktari wanaendelea kumfanyia matibabu, na bado hatujaruhusiwa kumuona. Kwa niaba ya wana Singida na Watanzania wote, nimetoa salaam za pole kwa mke wake, na bado nasubiri uwezekano wa kuweza kuonana naye usiku wa leo endapo madaktari wataruhusu,”amesema Nyalandu

Aidha Mbunge huyo amewataka Watanzania kiujumla kuendelea kumuombe Mbunge Tundu Lissu ili aweze kupona na kurejea nchini akiwa mzima wa afya njema

Hata hivyo, Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma na baadaye kusafirishwa kupelekwa jijini Nairobi Kenya kwa matibabu ambapo mpaka sasa yupo huko akiendelea kupata matibabu.

Video: Mbunge CCM amfuata Lissu, Balozi atamani kumpeleka Rais Magufuli Marekani
BAVICHA walibipu jeshi la polisi, wasema maombi yako palepale