Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameungana na viongozi wa Chadema kuweka kambi jijini Nairobi akisubiri ridhaa ya madaktari wa hospitali ya Nairobi kumpeleka Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu nchini Marekani kupata matibabu zaidi.

Nyalandu ambaye alifanikiwa kumuona Lissu na kuelezea hali yake, amesema kuwa madaktari wa hospitali ya Nairobi wamekuwa wazito kutoa ripoti maalum ya matibabu ya Lissu ili kumruhusu kumpeleka Marekani.

Mbunge huyo wa CCM ambaye amekuwa msitari wa mbele kushiriki kampeni ya kuchangisha fedha za kugharamia matibabu ya Lissu, ameonesha kuwa yeye ni mmoja kati ya watakaomsafirisha Lissu kwenda Marekani kupata huduma bora zaidi za matibau.

“Tumekuwa #NairobiHospital tukisubiri MADAKTARI watoe RIPOTI ya mwenendo wa MATIBABU ya Mh #TunduLissu kwa minajili ya kuwapatia MADAKTARI BINGWA wa Marekani na kuona uwezekano wa Mh #TunduLissu kupatiwa RUFAA kwa matibabu zaidi NJE., LAKINI bado KALAMU zao ni nzito kuandika RIPOTI hii siku ya tatu tangu tuahidiwe. Binafsi, nimerudi NAIROBI tangu JANA kushiriki maandalizi ya uwezekano wa kumhamishia Mh #TunduLissu Marekani kwa ajili ya huduma yenye ubora zaidi, endapo MADAKTARI wa #NairobiHospital wangeridhia. Kesho asubuhi nitarejea hospitalini kusikiliza kauli ya mwisho ya MADAKTARI kuhusu RIPOTI hiyo.” Nyalandu ameandika.

Lissu alijeruhiwa kwa risasi tano kati ya risasi zaidi ya thelathini alizoshambuliwa alipokuwa nyumbani kwake eneo la Area D mjini Dodoma, muda mfupi baada ya kutoka bungeni.

Video: Messi apiga nne Barcelona ikiibamiza Eibar 6-1
UNHCR yaitaka Congo-DRC kuimarisha ulinzi kwa wakimbizi