Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imezifungia nyimbo 15 za muziki wa kizazi kipya kuchezwa kwenye vyombo vya habari kwa madai ya kuwa nyimbo hizo hazikidhi vigezo kwa kukiuka maadili na kanuni za huduma za utangazaji  ya maudhui 2005.

Orodha hiyo ya nyimbo imetolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), na kusema kuwa zilitolewa na wasanii na kusambazwa katika vyombo mbalimbali vya utangazaji na mitandao ya kijamii bila kuzingatia kanuni na maadili kanuni zake.

Katika orodha hiyo ya nyimbo zilizofungiwa, nyimbo mbili zikiwemo za msanii anayefanya vizuri nchini Diamond Platinumz huku Ney wa Mitego akiwa amefungiwa nyimbo zake tatu ikiwemo nyimbo yake mpya aliyoitoa hivi kariuni inayojulikana kama ”Mikono juu”.

Zimetajwa nyimbo hizo kuwa ni

  1. Halleluyah – Diamond Platinumz.
  2. Waka Waka -Diamond Platinumz
  3. Kibamia – Rostam ( Roma Mkatoliki na Stamina na kumshirikisha Maua Sama)
  4. Pale kati patamu – Ney wa Mitego
  5. Hainaga Ushemaji – Manifango
  6. Iam Sorry JK – Nikki Mbishi
  7. Chura – Snura
  8. Tema mate tumchape – Madee
  9. Uzuri wako – Jux
  10. Nampa papa – Gigy Money
  11. Nampaga – Barnaba Classic
  12. Maku Makuz – Ney wa Mitego
  13. Nimevurugwa – Snura
  14. Bongo bahati mbaya – Young D
  15. Mikono Juu – Ney wa mitego

TCRA imesema nyimbo hizo zisirushwe katika chombo chochote cha habari nchini na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekiuka agizo hilo.

Nyika: Chirwa haendi Simba hata kwa dawa
Young Africans waipiga konzi Ndanda FC