Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Zanzibar, Tahuida Nyimbo amesema kuwa siku zote maamuzi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai hayajawahi kuwa ya kukurupuka.
 
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya sakata la Spika Ndugai kutoa agizo la CAG kufika mbele ya kamati ya Bunge ili kuhojiwa kwa madai ya kutoa kauli ya kulidhalilisha Bunge alipokuwa akihojiwa na kituo cha matangazo cha umoja wa mataifa akiwa nje ya nchi.
 
Amesema kuwa kutokana na jambo hilo, ni aibu kuona baadhi ya wanasiasa wakimkebei na kumdhalilisha Spika huku wakiwa wanatamani kukwamisha utendaji wake wa kazi.
 
Aidha, amesema kitendo cha Spika kumuita CAG kufika mbele ya kamati Ili kuhojiwa ni sahihi na hakuna sababu yoyote ya kutumia uamuzi wa Spika kisiasa na kutafuta ujiko kwa watu.
 
Hata hivyo, Nyimbo ameongeza kuwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watahakikisha wanapambana na wale ambao wanajaribu kuwapotosha Watanzania juu ya utendaji kazi za bunge na kuliona bunge kama halina watu makini.
 
Mbunge huyo amesema atahakikisha anasimamia ukweli katika serikali ya awamu ya tano sambamba na kutoa ushauri mwema kwa viongozi wa serikali kwa manufaa ya serikali na watanzania kwa ujumla wake.

Kanisa Katoliki lachangia vifaa Magereza mkoa wa Njombe
3.5 Bilioni kujenga makazi ya Askari Polisi