Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamebainika kuiibia maji Shirika laMaji Safi na Maji Taka, Dar es Salaam (DAWASCO) kwa mtindo unaofahamika kama ‘Nyoka’.

Wizi huo umebainishwa na Meneja wa Dawasco Kanda ya Ki-Dawasco ya Magomeni, Pascal Fumbuka wakati wa operesheni maalum inayoendeshwa katika eneo hilo. Amesema kuwa wamebaini wananchi wengi wamejiunganishia maji kiholela kwa kujitengenezea ‘laini’ na kisha kutumia mipira kuvuta maji kwenye majumba yao kwenda umbali mrefu, mtindo wa wizi walioupa jina la ‘Nyoka’.

Meneja huyo alisema kuwa mitaa iliyobainika kwenye kanda hiyo kutumia wizi huo ni Chama, Mkundunge zilizopo Sinza na Tandale. Wezi hao hujaza maji kwenye matanki yao na kisha kufanya biashara ya kuyauza, kinyume cha sheria na taratibu.

Amesema mbali na hatua za kisheria, wamechukua hatua ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya wizi huo wa maji na kuanzisha ‘Kiosk’ maalum kitakachowasaidia wakazi wa maeneo hayo kupata maji kwa urahisi.

Ndugu wa mgonjwa ampiga daktari Mtwara, Waanzisha Mgomo
'Bei za rushwa kwa wabunge zinajulikana'