Katika kile kimetajwa kama hatua kubwa kwenye tasnia ya utabibu, muuguzi mmoja kutoka nchini Uingereza ambaye alikuwa akipigania maisha yake hospitalini, aliamka baada ya kupoteza fahamu kwa siku 28.

Mwanamke huyo aliamka baada ya kupewa dozi moja ya dawa ya kuongeza hisia za kingono zijulikanazo kama (viagra).

Kulingana na vyombo vya habari vya Uingereza, Monica Almeida, (37), alilazwa hospitalini Novemba 9, 2021, baada ya kuambukizwa virusi vya COVID-19 mnamo Oktoba 19, 2021, licha ya kuchanjwa kikamilifu dhidi ya virusi hivyo.

Hata hivyo, baada ya kulazwa hospitalini, alipoteza hisia ya ladha na kunusa kwa siku nne kisha alianza kukohoa damu na viwango vyake vya oksijeni kushuka huku hali yake ikiendelea kudhoofika, na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi(ICU) cha Hospitali ya Lincoln County ambapo aliingia katika hali ya kutokuwa na fahamu mnamo November 6, 2021.

Akiwa amebakiwa na saa 72 tu kabla ya mashine yake ya kumsaidia kupumua kuzimwa, madakatri waliamua kumpa kipimo kikubwa cha viagra na hali yake ilianza kubadilika na hatimaye aliamka mnamo Disemba 14.

Inaripotiwa kwamba Almeida alitia saini ya kuwekwa katika hali ya kutokuwa na fahamu ya kimatibabu bila kulazimishwa ili kufanyia dawa hizo majaribio.

Picha ya mgonjwa akiwa amelazwa kwenye ICU. Picha: Getty Images.

Baada ya kurejesha fahamu, Almeida alisema, “Hakika Viagra ndiyo iliyoniokoa. Ndani ya masaa 48 ilifungua mawimbi yangu ya hewa na mapafu yangu yakaanza kujibu. Ikiwa unafikiri juu ya jinsi dawa inavyofanya kazi, huongeza mishipa yako ya damu. Nina pumu na mifuko yangu ya hewa ilihitaji usaidizi kidogo. “Nilimzulia mzaha kidogo mshauri baada ya kufika kwa sababu nilimfahamu. Aliniambia ni Viagra, nilicheka na kudhani anatania, lakini akasema ‘hapana, kwa kweli, umepata kipimo kikubwa cha Viagra,” aliongeza.

Hatimaye aliruhusiwa kwenda nyumbani mnamo Disemba 24,2021, kusherhekea siku kuu ya Krismasi pamoja na familia yake, hata hivyo, anatarajiwa kupona kikamilifu baada ya miezi kadhaa.

Kufuatia ufanisi huo, wanasayansi kote duniani sasa wanafanyia dawa hiyo majaribio kubaini iwapo inaweza kuongeza viwango vya oksijeni katika damu.

CAF: KIHARUSI CHA JOTO kilimvuruga Sikazwe
Juuko Murshid aitema The Cranes