Mlinzi mkongwe wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) Erasto Nyoni amerejea nchini akitokea Cameroon alikokuwa na kikosi hicho kushiriki michuano ya Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), sababu zikiwa hazijulikani, huku timu hiyo ikiwa bado ina mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Guniea.

Erasto amerejea nchini jana na amegoma kuzungumza na Wanahabari, huku akisema wako wazunginzaji wa urejeo wake huku michuano ikiendelea na sio yeye.

Mchezaji huyo kraka anayekipiga katika klabu ya Simba alikuwa mchezaji wa mwisho wa Stars kwenda nchini humo kuungana na kikosi hicho kilichokuwa kimetangulia.

Taifa Stars itacheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Gyinea keshokutwa Jumatano, na itahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya CHAN 2021.

Juzi Jumamosi Taifa Stars ilifufua matumaini ya kutinga hatua hiyo, baada ya kuifunga Namibia bao moja kwa sifuri, kupitia kwa kiungo mshambuliaji wa Young Aficans Farid Mussa Malik.

CHANZO: Clouds fm / Power breakfast

Afisa wa ngazi ya juu Korea Kaskazini akimbilia Korea Kusini
Mahakama yawaamuru polisi kuondoka nyumbani kwa Bobi Wine