Mchezaji kandanda wa zamani wa Taifa Stars na Yanga na Pan African, Jellah Mtagwa yupo kitandani akiugua kiharusi na anahitaji msaada wa matibabu pamoja na kujikimu kimaisha.

Mtagwa, ambaye hivi sasa amepooza nusu ya mwili wake, anaishi Manzese Friend’s Corner jijini Dar es salaam pamoja na familia yake akiwa hana msaada wowote kutokana na maradhi hayo na ufukara alio nao.

Wadau mbalimbali na mashabiki wa mpira wa miguu wameeleza kwa masikitiko yao kwa hali kama hiyo kumkumba aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya Taifa Stars ambaye picha yake iliwekwa kwenye stempu kutokana na mchango wake uliotukuka kwa nchi.

Aidha, wadau wa soka nchini na Watanzania wengi wanahoji endapo kama Shirika la Posta lilimlipa mchezaji huyo mrabaha wa kuwekwa sura yake mwenye stempu, na kama Shirikisho la Mpira nchini (TFF) wana taarifa zake na kama wanamsaidia kwa choche.

Hata hivyo, mpaka sasa umoja wa wachezaji soka wa zamani (UMSOTA) wameanzisha harambee ya kumsaidia mwenzao huyo kwa kuchangishana ili kumsaidia. ambapo tayari umoja huo umetoa ombi la msaada kwa wasamaria wema kumsaidi Jellah Mtagwa kwa kutangaza namba yake ya simu Namba 0755 693330 kwa yeyote atakayeguswa.

Wanaume tereza Kigoma wazua gumzo, LHRC yawakomalia
Mizani za kupima wagonjwa hospitaIini kufanyiwa marekebisho Njombe