Nyota wa zamani wa Ivory Coast, Emmanuel Eboue amelamba dili la ukocha wa vijana chini ya miaka 14 kwenye Klabu ya Galatasaray ya Uturuki.

Eboue ambaye amewahi kutamba na klabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Arsenal amepewa nafasi ya kuwa kocha msaidizi wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 14 (U-14) ya klabu ya hiyo.

Aidha, Galatasaray imemtaka Eboue kushughulikia leseni yake ya kufundisha soka ili aweze kuanza kibarua rasmi ndani ya timu hiyo ili kuokoa hali yake ya kimaisha.

Klabu hiyo inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu soka ya Uturuki, imemwahidi mshahara mnono ili kusaidia kurejesha hali yake nzuri ya kimaisha,

Hata hivyo, Eboue amejikuta kwenye wakati mgumu wa maisha baada ya mahakama kuamuru mali zote kukabidhi kwa mke wake. ambaye waliachana huku akiwa ameandika jina la mkewe katika sehemu kubwa ya mali zake ikiwemo nyumba za kifahari alizokuwa amezinunua kutokana na malipo yake kama mchezaji.

Eminem aukwapua mwaka 2017, avunja rekodi za Billboard
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 26, 2017