Pengine mpango wa mwanamuziki Maua Sama kuhusu ujio wa wimbo wake mpya anaotarajia kuachia siku za usoni utakaokuwa na jumla ya dakika 23 utaweka rekodi ya wimbo mrefu zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya muziki wa Bongo fleva.

Kufuatia maandalizi hayo, Maua Sama amefunguka mapya kuhusu matayarisho ya wimbo huo ikiwamo kumtaja Executive producer wa mradi huo wa wimbo wenye dakika 23, ambaye ni mwanamuziki na mbunge wa Muhezi Hamis Mwinjuma maarufu MwanFa.

“Dear GODFATHER, Hon Hamis Mwinjuma , (MP) MwanaFa kwanza nikushukuru kwa kila kitu. Uliamini katika Kipaji changu na kufanya mziki kuwa ajira yangu. UMENIPAMBANANIA Sana.

Katika kipindi chote hukuchoka na uliamini nitafanya uwe proud kwa maamuzi yako ya kunieleta mjini.

Kwenye track ya Dk 23 za CINEMA ukaamua kutumia Pesa zako, Ubunifu, muda wako mbali na majukumu magumu ya kuwatumikia Wananchi wa Muheza, na mpaka kuamua usitoe Ngoma mpaka nikamilishe project Yangu. Asante sana” ameandika Maua

Licha ya kumshukuru rapa na Mbunge huyo, Maua pia amemtaja mtayarishaji mahiri wa muziki nchini Hermy B kama muongozaji wa mradi huo ‘Music Director” kwa kuweka kidogezo cha kionjo cha mtayarishaji huyo.

“Kwenye Track hii ya Hermy B 23 Minutes, Zilikuwa Dk 49 lakini zikapunguzwa mpaka kufika 23! Kuna wakati nilijua hatuwezi kumaliza hii Kazi Maana kila siku yalikuwa yanaletwa makosa mapya.

Yaliyonilazimu lazima niende tena studio S/O to my Brother from another Mother Hermy B. wakati unaendelea kuEnjoy na video ya Baba Jeni, Ngoma yetu ya Dk 23 iko tayari” ameongeza.

Maua ameyasema hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa Instagram akibainisha dhahiri namna MwanaFa alivyojitoa kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha mafanikio ya mradi huo yanatekelezeka kwa asilimia mia moja

Aliyemuuzia Mac Miller dawa za kulevya na kumsabishia kifo atupwa jela miaka 17
Jonas Mkude, Clatous Chama kuikosa Azam FC