Nyumba 20 zimeteketea kwa moto na nyingine 10 zimeharibiwa baada ya moto kushika jengo moja huko mashariki ya London nchini Uingereza.

Moto huo ulienea katika ghorofa zote sita katika jengo hilo lililopo eneo la De Pass Gardens, Barking, majira ya saa tisa na nusu mchana majira ya Uingereza.

Aidha, takriban wazimamoto 100 walifanya kila liwezekanalo kuuzima moto huo kwa zaidi ya masaa mawili, ambao hatimaye walifankiwa kuuzima majira ya saa kumi na mbili jioni, ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakikajajulikana.

Mwanamme mmoja na mwanamke mmoja walitibiwa kwa kuathiriwa na moshi waliokuwa wanauvuta wakati ajali hiyo ya moto ilipotokea. ambapo walipatiwa matibabu katika eneo la ajali na hakuna taarifa nyingine juu ya majeruhi.

LIVE: Yanayojiri Bungeni Jijini Dodoma
Viongozi wa umma kutoka mikoa 12 kuchunguzwa

Comments

comments