Jeshi la Polisi nchini Kenya limeanza kufanya uchunguzi kufuatia kuwepo kwa taarifa za kupigwa risasi nje ya nyumba ya moja ya kiongozi wa upinzani National Super Allience (NASA), Kalonzo Musyoka.

Tukio hilo limetokea katika makazi ya kiongozi huyo yaliyopo eneo la Karen, jijini Nairobi, ambapo imeelezwa hakuna mtu aliyejeruhiwa.

Taarifa Zaidi zimeeleza kuwa mtu asiye fahamika alipiga risasi hewani katika eneo hilo kisha kutokomea kusikojulikana.

Hata hivyo, tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya kiongozi huyo kushindwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa kiongozi mwenza wa upinzani Raila Odinga katika viwanja vya Uhuru park.

Mchakato wa kupata cheti kufanyika ndani ya siku 30
Wema kuja kivingine Juni 30, 2018, Diamond amsapoti

Comments

comments