Kundi la nzige limevamia nchi ya kidemokrasia ya Congo (DRC) ikiwani mara ya kwanza kwa wadudu hao kuonekana katika Taifa la Afrika ya kati tangu mwaka 1944 ambapo shirika la chakula Duniani (FAO) jana lilionya juu ya tishio la njaa katika mataifa ya Afrika mashariki  baada ya kuvamiwa na nzige hao.

Umoja wa mataifa umesema nzige hao waharibifu pia wameonekana Djibout na Eritrea katika siku za karibuni wamefika Sudani kusini nchi ambayo takribani nusu ya watu wake wanakabiliwa na njaa baada ya miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa mujibu wa shirika la habari la DW likinukuu taarifa ya pamoja ya viongozi wa mashirika ya kimataifa iliyotolewa jana jioni imefananisha kundi hilo la nzige kama janga lililozungumziwa kwenye biblia na linalokumbushia hatari inayoikumba ukanda huo.

Msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Stephane Dujarric akiwa mjini New York ametoa wito wa kasi ya utekelezaji kupitia ufadhili uliotolewa na Fao wa dola za Marekani 76 millioni wa kupambana na wadudu hao.

Ikumbukwe kuwa Kenya, Somalia na Uganda zimekuwa zikipambana na wadudu hao waharibifu ambao katika baadhi ya maeneo historia inaonyesha kwamba walishuhudiwa miaka 70 iliyopita.

 

Rugemarila aruhusiwa kuwasilisha hoja za kuachiwa huru
Saudi Arabia: Yazuia safari za kidini nchini humo