Msemaji wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa (FAO), ametoa wito wa kutolewa kwa msaada ili kukabiliana na athari za nzige ukanda wa Afrika mashariki, kama vile ukosefu wa chakula, utapiamlo na kuathirika kwa mfumo wa maisha ya kila siku.

Shirika la FAO limesema Ethiopia, Kenya na Somalia zinapitia wakati mumu kukabiliana na makundi ya nzige ambako hakujawahi kutokea hapo kabla kunakoathiri mazao ya kilimo,

Shirika hilo linahofia kwamba idadi ya nzige hao huenda ikaongezeka mara 500 zaidi ifikapo Juni mwaka huu.

Shirika hilo limeondeza kuwa, Ethiopia na Somalia hazijawahi kushuhudia nzige wa aina hiyo kwa kipindi cha miaka 25 huku Kenya ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 70.

Sudani Kusini na Uganda pia zipo katika hatari ya kuingiliwa na nzige hao ambao wanaendelea kuongezeka na kusambaa.

Uhaba wa mchanga Zanzibar, tishio kisiwa kutoweka
KCMC yatengeneza hewa ya kuhifadhi mbegu za uzazi