Rais wa Marekani, Barack Obama amemwaga machozi wakati akitoa hotuba kuhusu uanzishwaji wa sheria ya kudhibiti matumizi ya silaha za moto.

Hotuba hiyo ya Obama ilijaa hisia kali na maneno yaliyogusa nyoyo za wananchi wengi akizungumzia mauaji ya raia wengi wa nchi hiyo kutokana na umilikaji wa silaha za moto bila kuweka udhibiti wa kutosha.

Katika mapendekezo yake, Obama alieleza hakatazi mtu kumiliki silaha za moto bali anataka mtu anayetaka kumiliki silaha hizo kufuatiliwa maombi yake ikiwa ni pamoja na kuangaliwa kumbukumbu ya uhalifu, kupimwa akili na sababu za umiliki wa silaha za moto.

Alisema kuwa suala la kumiliki silaha lilikuwa limeliteka bunge la Congress lakini halitaweza kuteka nyara Marekani yote kwa kuzingatia kuwa kipindi hiki ni kipindi ambacho mauaji ya kutumia silaha yamechukua maisha ya wamarekani wengi kuliko ajali za barabarani.

Obama anatarajiwa kuweka hadharani mikakati na hatua zitakazochukuliwa kutokana na matumizi mabaya ya silaha za moto nchini humo.

Hata hivyo, Chama cha wafanyabiashara za silaha nchini Marekani kilichoanzishwa mwaka 1871 chenye jukumu la kutetea haki za kumiliki silaha na kufuatilia usalama wa matumizi ya silaha za moto nchini humo, kimeikosoa hotuba ya Obama na kudai kuwa mapendekezo yake hayatazuia mauaji ya halaiki.

 

 

Rais Wa FC Barcelona Achukizwa Na Taarifa Za Lionel Messi
Michael Carrick Ashangazwa Na uvumi Dhidi Yake