Rais wa Marekani, Barack Obama ameamuru kufanyika kwa marejeo ya kina kuhusu tuhuma za wadukuzi wa Urusi kuingilia uchaguzi wa Urais uliompa ushindi Donald Trump dhidi ya Hillary Clinton.

Mshauri wa Rais Obama wa mambo ya ugaidi na ulinzi wa ndani, Lisa Monaco jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa  kiongozi huyo amechukua uamuzi huo ili kupata ukweli wa kilichofanyika hasa katika majimbo matatu muhimu yaliyompa ushindi Trump.

“Tumepitia kwenye kizingiti kipya na tumeamua kuchukua nafasi kuhusu hilo, kufanya marejeo, kufanya baadhi ya mambo kujua kilichotokea baada ya kitendo, kuelewa kilichotekea na kutoa somo tulilojifunza,” alisema Monaco.

Tamko hilo la Obama limekuja wakati ambapo kumekuwa na vuguvugu kutoka kwa wanaharakati na wataalamu wa kufanya majumuisho ya mahesabu kutaka kurudiwa kwa uhesabuji kura katika majimbo matatu muhimu yaliyompa ushindi Trump.

Rais Obama anatarajiwa kukabidhiwa ripoti hiyo kabla hajakabidhi rasmi ofisi kwa Rais Mteule, Trump Januari 20 mwakani. Monaco ameeleza kuwa ripoti hiyo itawekwa wazi kwenye Bunge la Congress lakini hakueleza kama itawekwa wazi pia kwa umma.

Magufuli atoboa siri ya kufuta shamrashamra za uhuru mwaka jana, kuruhusu mwaka huu
Waziri Mkuu apokea taarifa za Faru John, ataka uchunguzi zaidi