Katika kuonyesha kuwa Marekani haijafurahishwa na kitendo cha Urusi cha kufanya udukuzi wa siri katika uchaguzi wa Marekani uliompa ushindi Rais mteule wa nchi hiyo Donald Trump, Obama ameamuru kufukuzwa kwa wanadiplomasia 35 wa Urusi kufuatia tuhuma hizo.

Rais Obama amesema kuwa alimuonya Rais Putin wa Urusi kuhusu udukuzi wa kura katika uchaguzi huo na kuwadhalilisha maafisa wa Marekani  na ametahadhalisha  kuchukua hatua kali endapo Urusi itaendelea na tabia hiyo.

Aidha, amesema kuwa wamarekani wote wameshtushwa na vitendo vya Urusi, hii ikionekana kama njia ya kumjibu mrithi wake Donald Trump ambae amesema kila mtu aishi maisha yake.

Hata hivyo Urusi imekanusha tuhuma za kufanya udukuzi huo kwa kutumia mfumo wa mtandao wa chama cha Democratic,huku ikisema kuwa italipiza kwa kitendo ilichofanyiwa na Marekani.

Video: Darassa afunguka kuhusu Hip Hop, asema heshima haitengenezwi na mtu mmoja
Diamond atikisa Australia, wimbo wake wavunja rekodi ya mwaka