Chama cha Mpira wa kikapu Nchini Marekani (NBA) kimetangaza Rais Mstaafu wa nchi hiyo, Barack Obama kuwa sehemu ya wamiliki wa mradi wa ‘NBA Africa’.


Rais Obama anamiliki sehemu ndogo ya hisa za mradi huo ambapo kitambo alikusudia kutumia fedha zitakazopatikana kufadhili programu ya Vijana na Uongozi barani Afrika ya Taasisi ya Obama( Obama foundation).

Obama atasaidia kuendeleza juhudi za majukumu ya kijamii za mradi huo barani Afrika hususani programu zinazosaidia kukuza usawa wa kijinsia na Uchumi Jumuishi.

‘NBA Africa’ inaendesha na kusimamia biashara ya mpira wa kikapu barani Afrika ikiwemo Ligi ya Mpira wa Kikapu Barani Afrika (BAL) inayohusisha timu 12 za juu kutoka nchi za Afrika.

Rais Samia afanya uteuzi
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 2, 2021