Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegon Obasanjo, amemshauri Rais wa sasa, Muhammad Buhari, asigombee muhula mwingine wakati wa uchaguzi wa 2019.

Obasanjo ambaye aliwahi kuiongoza Nigeria mwaka 1999 hadi 2007, amesema kuwa Rais Buhari hana ufahamu wa masuala ya uchumi, na amekuwa akiteua wasaidizi wake kwa misingi ya upendeleo.

Aidha, Buhari amekuwa madarakani tangu Mei 2015, baada ya kumshinda Goodluck Jonathan ambapo Obasanjo pia amemshauri kiongozi huyo kupumzika masuala ya siasa kutokana na hali yake ya afya.

Hata hivyo, Buhari mwenye umri wa miaka 75, alikaa nchini Uingereza kwa zaidi ya siku 100 kwa vipindi tofauti tofauti akipatiwa matibabu kwa ugonjwa ambao haujawekwa wazi.

Museven amsifu Trump
Magazeti ya Tanzania leo Januari 24, 2018