Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amesema tayari ameanza mapambano ya kumuondoa madarakani Rais, William Ruto akisema alikuwa na kura za kutosha katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2022.

Odinga ambaye alikuwa akiwahutubia wafuasi wake nchini humo, amesema alishinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwa zaidi ya kura milioni mbili, na kwamba amebaini hayo baada ya wataalamu wa data kuyachunguza matokeo.

Raila Odinga (kushoto) na William Ruto (kulia). Picha ya DN.

Hata hivyo, matokeo rasmi ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), yalionesha kuwa Ruto alipata kura milioni 7.18 huku Odinga akipata kura milioni 6.94 na hivyo Ruto kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo.

Mkutano huo, unafanyika ikiwa ni siku chache baada ya Odinga kusema alimshinda Rais Ruto kwenye uchaguzi mkuu uliopita, huku akisema hataogopa chochote kwenye azma yake baada ya kunyang’anywa ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Hata hivyo, mapema hapo jana Januari 23, 2023 Rais Ruto alisema hatafumbia macho vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyopangwa kufanywa na wapinzani wake.

Vijana wabuni mradi mabegi ya Nishati jua
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 24, 2023