Kiongozi wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya, National Super Alliance (NASA), Raila Odinga ameahirisha mkutano wake aliokuwa amepanga kufanyika mapema hii leo kwaajili ya kutoa mwelekeo wa muungano huo kufuatia kushindwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Odinga aliahidi kutangaza hatua ambazo angechukua mapema hii leo mara baada ya kushindwa na mpinzani wake Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika hivi karibuni.

“Tunasikitika sana kwamba mashauriano yetu yanachukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa na Nasa kwa hiyo hawataweza kuwahutubia Wakenya kama walivyotarajia leo siku ya jumanne na badala yake hotuba itatolewa kesho,”amesema Wakala wa Nasa, Musalia Mudavadi.
Aidha, Rais Kenyatta alitangazwa kuwa mashindi kwa kura 8,203,290 huku mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo, Raila Odinga akipata kura 6,762,224 kitu ambacho kilipingwa vikali na muungano wa NASA kwa madai kuwa matokeo yamechakachuliwa.
Hata hivyo, Tume ya uchaguzi inchini Kenya imesema kuwa hakuna udukuzi wowote uliofanyika katika uchaguzi huo hivyo matokeo yalikuwa sahihi hivyo, uhuru Kenyatta ni mshindi halali.

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 16, 2017
Prof. Ole Gabriel: Vyombo vya habari shirikianeni na BAKITA