Timu ya wanasheria wa mgombea urais wa Azimio, Raila Odinga tayari imewasilisha nakala ya kielektroniki ya ombi la kupinga ushindi wa Rais Mteule William Ruto.

Kwa mujibu wa sheria, timu hiyo ya mawakili ina masaa nane kuwasilisha pingamizi lao dhidi ya ushindi wa Naibu Rais William Ruto katika Uchaguzi uliofanyika Agosti 9, 2022.

Seneta mteule wa Makueni, Dan Maanzo, mmoja wa mawakili katika timu ya wanasheria, amethibitisha kuwa kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa rasmi kwa njia ya kielektroniki Jumatatu asubuhi katika Mahakama ya Juu.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha CNN, Maanzo alisema kuwa “Tuna ombi kali na tunatumai kuwa litatekelezwa,”

“Tunaomba mahakama iamue kama katiba ilifuatwa katika kutangaza matokeo ya urais. Ikiwa haikuwa ndani ya katiba, basi ni batili.” amesema

Hata hivyo Mahakama ya Juu ina siku 14 kuanzia Jumatatu kusikiliza kesi ya Odinga na kutoa uamuzi.

Muungano wa Azimio La Umoja (Aspiration to Unite), wa Odinga ulidai ulikuwa na ushahidi wa kutosha katika ombi hilo kuthibitisha utovu wa nidhamu wa tume ya uchaguzi baada ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9 ambao ulisababisha ushindi mdogo wa Naibu Rais William Ruto.

Iwapo majaji hao saba, watatoa uamuzi na kumuunga mkono Odinga mwenye umri wa miaka 77, wanaweza kuagiza kura zihesabiwe upya, uchaguzi mpya au kumpa Odinga nafasi ya urais.

Wananchi 'wajiweka rehani' ajali ya Lori la mafuta
Kenya: Odinga atinga Mahakamani 'kibabe' na Lori la ushahidi