Kiongozi wa upinzani nchini Kenya kupitia NASA, na Rais wa watu Raila Amollo Odinga ametoa tamko kuhusu yeye kuhamia Ikulu na amesema kuwa hana mpango wowote wa kupambana na Serikali ya Uhuru Kenyatta.

Raila amesema kuwa Uhuru Kenyatta anaweza kuendelea kukaa Ikulu kwa amani lakini amesisitiza kuwa Wananchi wa Kenya hawamtambui kama Rais wa nchi hiyo.

Raila amedai kuwa Kenyatta hana kibali cha watu na ametangaza rasmi kuwa Agosti mwaka huu, 2018  kufanyika uchaguzi mkuu mpya.

Hayo yamezungumzwa pindi alipokuwa akihojiwa na BBC.

“Hatutamtoa Uhuru Kenyatta Ikulu anaweza kuendelea kukaa kwa amani, lakini hatuutambui Urais wake kwa sababu uko kinyume, tunataka uchaguzi mwingine na kwa mujibu wa ratiba yetu utakuwa Agosti mwaka huu”, amesema Raila Odinga.

Hivi karibuni kiongozi huyo wa upinzani nchini Kenya alijiapisha na kuwa Rais wa watu, akisema yeye ndio chaguo la watu kuwaongoza na sio Uhuru Kenyatta.

Dkt. Abbas afunguka kuhusu mamilioni ya JPM
Mlinga amfumua Ndalichako kuhusu Shule za serikali kushika mkia