Kiongozi wa Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza rasmi kuwa muungano wake wa National Super Alliance (NASA) utawasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne wiki iliyopita.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Nairobi, ambapo amesema kuwa ingawa muungano huo ulikuwa umeapa kutowasilisha kesi mahakamani kwa kipindi hiki, lakini wameona kuwa ni heri kufanya hivyo ili kuweza kufichua maovu yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu.

“Tumeamua kwenda mahakamani kufungua kesi ili tufichue jinsi kura zilivyokuwa zikichakachuliwa, tuwaonyeshe Wakenya uovu uliokuwa ukifanyika wakati wa upigaji kura,na kupelekea kumpa ushindi Uhuru Kenyatta,” amesema Odinga

Aidha, Odinga amesema kuwa mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo kuvurugwa kwaajili ya kumnufaisha, Uhuru Kenyatta ambapo kulikuwa na pengo dogo kati yake na mpinzani wake.

Hata hivyo, ameongeza kuwa udukuzi huo una uhusiano mkubwa na mauaji ya meneja wa teknolojia katika tume hiyo Chris Msando ambaye aliuawa wiki moja kabla ya uchaguzi huo kufanyika.

 

Andre Schurrle Hadi Mwezi Septemba
Kamishna wa tume ya uchaguzi Kenya azuiliwa Uwanja wa Ndege