Kiongozi wa Chama cha Upinzani cha ‘Orange Democratic Movement (ODM)’ cha Kenya, Raila Odinga ameomboleza kifo cha Rais Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya 3, Benjamin Mkapa kilichotokea usiku wa kumkia leo kwa kumkumbuka kwa mengi ikiwepo alivyosuluhisha vurugu baada ya uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo 2007 – 2008.

Odinga ameandika, “Kenya tunabakiwa na kumbukumbu kubwa kwa namna alivyohusika pamoja na Dkt. Kofi Annan (Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa) na Graca Machel kusaidia nchi hii kurudi katika amani baada ya vurugu kufuatia Uchaguzi Mkuu wa 2007-2008″

Ameongeza kuwa licha ya upatanisho huo pia Mkapa anakumbukwa kwa kuwa kiongo cha Pan Africanism na ushirikiano wa kusini mwa afrika.

“Mkapa alikuwa rafiki mkubwa wa watu wa Kenya, muumini mkubwa wa Pan Africanism na muamini mkubwa wa ushirikiano wa Kusini-Kusini” Ameandika Ondinga kwenye ukurasa wake wa Tweeter

Klabu za VPL zamlilia Mkapa
Katwila aahidi kujiuzulu Mtibwa Sugar