Kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Crystal Palace kilikua shubiri kwa wachezaji wa Watford katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la FA uliochezwa jana kwenye uwanja wa Wembley jijini London, lakini kwa mshambuliaji Odion Ighalo ilikua shubiri zaidi kufuatia kifo cha baba yake mzazi.

Ighalo ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Watford kilichokua kikisaka nafasi ya kuelekea kwenye mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya kombe la FA, alithibitisha ukweli wa taarirfa za msiba wa baba yake mapema hii leo.

“Nimempoteza baba mapema hii leo,” Amesema Ighalo

“Alikua analalamika kuhusu maumivu wa mwili dakika chache kabla ya kwenda kulala, na baadae mida kama ya saa nane usiku alifikwa na umauti.”

“Inauma sana kumpoteza baba yangu kipenzi”. Aliongeza Ighalo

Taarifa hizo zimepokelewa kwa uchumngu mkubwa na mashabiki wa soka wa klabu ya Watford pamoja na wale wa mshambuliaji huyo, ambaye kwa hakika atakua na maumivu makali moyoni mwake hasa ikizingatiwa tukio la kifo cha baba yake limetokea saa kadhaa baada ya kupoteza mchezo wao muhimu wa hatua ya nusu fainali.

Kwa msimu huu Ighalo amefanikiwa kufunga mabao 16 katika michezo 35 aliyocheza mpaka sasa.

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI TENA
Juventus Watetea Ubingwa Wa Scudetto Kwa Mbwembwe