Waandamanaji wenye hasira nchini Burkina Faso wameushambulia ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Ouagadougou wakimuunga mkono kiongozi mpya wa kijeshi, Ibrahim Traore na kuishutumu Ufaransa kwa kumhifadhi rais wa mpito Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, ambaye amepinduliwa.

Hali ya sintofahamu imeendelea huko Ouagadougou, baada ya taarifa ya jeshi kusema halitambui mapinduzi hayo na kwamba pia hawajui alipo Damiba na mamlaka za Ufaransa zimekanusha kuhusika na tukio hilo huku ikisema usalama wa raia wake ndio kipaumbele chake kufuatia mapinduzi ya kijeshi.

Waandamanaji nje ya jengo la Ubalozi wa Ufaransa nchini Burinafaso. Picha na cbc.ca

Hata hivyo, waandamanaji hao wameendelea kupaza sauti kwa hasira kwa kauli mbiu za kuipinga Ufaransa huku wakisema, “Hatuitaki Ufaransa tena tunaitaka Urusi na ndiyo maana tunashikilia bendera tatu za Urusi, Mali na Burkinabe, Damiba ameshindwa na wananchi hawana furaha.”

Awali, Damiba alikuwa ameahidi kukabiliana na ghasia za wanajihadi lakini wakosoaji walimtuhumu kuwa karibu sana na Ufaransa ambayo inadumisha uwepo wa kijeshi katika eneo hilo, ambapo Msemaji wa Ufaransa Anne-Claire Legendre alisema alilaani ghasia dhidi ya ubalozi huo na kusema kuwa maandamano hayo ni kampeni ya kupotosha habari dhidi ya Ufaransa.

Bil. 2.7 zatolewa 'kupiga jeki' utafiti Tiba Asili
Zaidi ya Wanaume 500 waripotiwa kunyimwa unyumba, kupigwa