Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo ameileza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kuanzisha kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida za Muungano.

Amesema hayo jijini Dodoma wakati wa Kikao cha Kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa Kamati hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa Kamati hiyo katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Amesema, Mungano wa Tanganyika na Zanzibar umeendelea kuimarika kutokana na upendo na mshikamano wa wananchi na hivyo kuufanya uwe wa kipekee duniani na kwamba Serikali itafanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Pamoja na yale masuala 22 ya Muungano kwa mujibu wa Katiba ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika.

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika Kikao cha Kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa Kamati hiyo Ofisi za Bunge jijini Dodoma.

“Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia wataalamu wetu itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Muungano na faida zake kwa jamii kupitia vyombo vya habari na maadhimisho mbalimbali. Aidha, ili kuboresha utoaji elimu kwa umma, Ofisi imeandaa Kitabu cha Historia ya Muungano kitakachotumika kuelimisha umma
kuhusu faida za Muungano kiuchumi, kijamii na kiutamaduni,“ amesema Jafo. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Joseph Mhagama pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wamepongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa taarifa nzuri na kuongeza kuwa upo umuhimu wa kutoa ufafanuzi kuhusu hoja za Muungano zilizotatuliwa ili wananchi wapate uelewa kuhusu mambo gani yaliyopata ufumbuzi kwa pande zote mbili za Muungano.

Serikali yazindua mradi wa ghala uhifadhi mazao ya Chakula
Esther atoa siri iliyompandisha cheo kazini